Manchester,England.
Mlinda mlango Victor Valdes 33 anatarajiwa
kuanza kuidakia Manchester United katika mchezo wa Kombe la FA Raundi ya
Nne dhidi ya Cambridge United Ijumaa usiku dimba la Abbey
.
.
Mlinda
mlango huyo wa zamani wa Barcelona, ataidakia Manchester United kwa mara ya
kwanza tangu atue klabuni hapo hivi karibuni dhidi ya timu hiyo ya daraja la chini ya Cambridge, kwenye uwanja wake wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 8,100.
Valdes amesaini mkataba wa miezi 18ni chaguo la pili klabuni hapo nyuma ya raia mwenzake wa Hispania David De Gea.
0 comments:
Post a Comment