Kiungo wa klabu ya Newcastle United Muargentina Jonas Gutierrez (31) jumatatu hii alirejea dimbani kwa mara ya kwanza na kukifungia cha U21 cha klabu hiyo goli la kusawazisha katika mchezo wa kirafiki dhidi ya klabu ya daraja la kwanza ya Shellfield Wednesday.
Gutierrez aligundulika kuwa ana kansa ya korodani mwezi
mei mwaka 2013 kufuatia jeraha alilolipata baada ya kugongana na mlinzi wa zamani wa Arsenal Bacary Sagna.
Gutierrez ambaye amebakiza miezi sita kumaliza mkataba wake alijiunga na Newcastle mwaka 2008 akitokea klabu ya Real Mallorca ya Hispania akielezea furaha yake baada ya kumalizika kwa mchezo huo amesema
"Nimecheza michuano mingi mikubwa.Nimecheza kombe la dunia lakini nikipata tena nafasi kukichezea kikosi cha wakubwa cha Newcastle basi nitakuwa ni mwenye furaha kupindukia"
"Nimekuwa nikilia machozi pindi mashabiki wa klabu hii wanapokuwa wakilitaja jina langu.Nahitaji tena kucheza mbele yao niwaambie asante kwa kuniunga mkono katika kipindi chote cha ugonjwa wangu"
0 comments:
Post a Comment