Tiote:Habari zinasema klabu ya Arsenal imefanya mazungumzo na wakala wa kiungo wa Newcastle Cheick Tiote 28 kwa ajili ya kumsajili januari hii.Tiote inataka mshahara wa £80,000 na mkataba wa miaka mitatu na nusu.
Quadrado:Klabu ya Chelsea imeripotiwa kuanza mazungumzo ya kumnasa nyota wa klabu ya Fiorentina raia wa Colombia Juan Quadrado mwenye thamani ya £28m.
Drimic:Klabu ya Bayern Leverkusen imeripotiwa kutaka mshambuliaji wa klabu ya Tottenham Roberto Soldado na katika kuharakisha usajili huo iko tayari kutoa pesa na mshambuliaji wake Mswisi Josep Drimic.
Kane:Klabu ya Tottenham inajipanga kumpunguzia mzigo wa kufunga magoli nyota wake Harry Kane kwa kusajili washambuliaji wengine wapya.Wanaotajwa sana ni Jay Rodriquez na Carlos Bacca.
Cavani:Mshambuliaji wa klabu ya Psg Edinson Cavani ameonyesha kupendelea zaidi kuhamia klabu ya Arsenal kuliko vilabu vya Manchester United na Liverpool hapo majira ya joto.
Paulista:Taarifa kutoka vyombo vingi vya habari nidai kuwa klabu ya Arsenal iko katika hatua nzuri ya kumnasa mlinzi wa Villarreal Gabriel Paulista 24 baada ya kukubali kutoa ada ya £10m.
0 comments:
Post a Comment