728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, January 15, 2015

    TAARIFA ZOTE MUHIMU ZA USAJILI ULAYA ZIKO HAPA ...KARIBU

    Strootman:Raisi wa klabu ya As Roma James Pallotta amesema klabu ya Manchester United inapaswa kutoa dau kubwa kama kweli  inataka kumsajili kiungo wake  Kelvin Strootman.

    Paulinho:Klabu ya Juventus imeripotiwa kuanza mazungumzo ya kumsajili kiungo wa klabu ya Tottenham Mbrazil Paulinho (27).Paulinho amejikota akisota benchi baada ya kupokonywa namba na viungo Ryan Mason na Nabir Bentareb.

    Brozovic:Klabu ya
    Arsenal imeripotiwa kuwa imepeleka ofa ya kati ya £6-8m kwa ajili ya kumsajili kiungo mahiri wa klabu ya Dynam Zagreb Marcelo Brozovic (22)

    Pogba:Klabu ya Real Madrid inajipanga kutoa kitita cha £78m kwa ajili ya kumnasa kiungo wa klabu ya Juventus Paul Pogba (21) hii ni baada ya wakala wake Mino Raiola kusema mteja wako atahama msimu ujao.

    Zouma:Klabu ya Inter Milan imeripotiwa kuanza kumnyatia mlinzi wa Chelsea Kurt Zouma (19) ili imsajili kwa mkopo mpaka mwishoni mwa msimu.

    Song:Klabu imeingia katika mchuano mkali na klabu ya Westham kwa ajili ya kuipata saini ya kiungo Alex Song (27) toka klabu ya Barcelona.Song kwa sasa yuko kwa mkopo katika klabu ya Westham.

    Januzaj:Kocha wa klabu ya Manchester United Luis Van Gaal ameripotiwa kuwa tayari kumruhusu kinda wa klabu hiyo Adnan Januzaj (19) aondoke kwa mkopo mwezi huu.

    Perrin:Klabu ya Saint Etienne imeitaka klabu ya Arsenal kuwa mpaka ijumaa iseme rasmi kama kweli inamtaka mlinzi/kiungo wake Loic Perrin (29) vinginevyo haitosikiliza ofa yoyote toka klabu hiyo ya London.

    Gomis:Kocha wa klabu ya Swansea City Garry Monk ameiambia klabu ya Arsenal kuacha kujisumbua kumtaka mshambuliaji wake Batefimbi Gomis (29) kwa kuwa hauzwi.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: TAARIFA ZOTE MUHIMU ZA USAJILI ULAYA ZIKO HAPA ...KARIBU Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top