Mshambuliaji wa Yanga, Mrisho Ngasa amelizua jipya baada ya kubainika kuikimbia timu hiyo na kwenda Afrika Kusini kufanya majaribio katika klabu moja ya huko.
Awali, Ngasa alikosekana katika timu hiyo kwa wiki moja na uongozi wa timu hiyo ukieleza kwamba anamuuguza ndugu yake ambaye ni mgonjwa.
Katibu wa Yanga, Dk Jonas Tibohora alisema Ngasa aliondoka katika timu hiyo akiomba ruhusa maalumu ya kumuuguza ndugu yake, lakini uongozi wao umepata taarifa kwamba yuko Afrika Kusini
akisaka timu ya kumsajili bila ya ruhusa ya klabu yao.
Tibohora ambaye kitaaluma ni daktari wa Sayansi ya Michezo alisema taarifa hizo walizipata kutoka kwa baadhi ya wadau
wa klabu yao ambao wamemwona mshambuliaji huyo nchini humo huku klabu inayotajwa kwamba ndiyo inataka kumsajili ni Free State Stars, ambayo iliwahi kumfanyia majaribio mwaka jana.
Alisema kwa sasa wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo na endapo watabaini ukweli katika utovu huo wa nidhamu wa mshambuliaji huyo, mara baada ya kurudi watakutana naye huku
pia kuna uwezekano wa kuishtaki klabu ambayo ibainika amekimbilia.
“Alikuja kwangu akaomba ruhusa
kwamba anamuuguza ndugu yake, kibinadamu hatukuweza kumzuia,tukamkubalia, lakini taarifa tulizopata ni kwamba hayuko nchini kitu ambacho
kilitushtua na hata tulipokuwa
tunamtafuta kutaka kujua maendeleo ya mgonjwa wake, hatukuwa tunampata,”alisema Tibohora.
“Awali nilimshtukia Ngasa wakati
anaomba ruhusa, alitaka pia tumpatie barua ya kwenda kushughulikia pasi yake
ya kusafiria, nilijiuliza kuna uhusiano gani kati ya mgonjwa na pasi ya kusafiria, sikupata majibu, tunaendelea na uchunguzi wa hilo,” aliongeza
0 comments:
Post a Comment