London,England.
Klabu ya Arsenal imeibuka na ushindi wa goli 3-2 dhidi ya klabu ya Brighton & Hove Albion katika muendelezo wa michezo ya kombe la FA jioni ya leo.
Arsenal ikicheza katika dimba la ugenini la Amex ilipata goli lake la kwanza kupitia kwa Theo Walcott huku Mesut Ozil akifunga la pili kabla ya Thomas Rosicky kufunga la tatu.
Magoli ya wenyeji Brighton yalifungwa na Chris O’Grady aliyefunga la kwanza kabla ya Sam Baldock kufunga la pili.
Matokeo mengine ya FA ni kama ifuatavyo...
Aston Villa 2-1 AFC Bournemouth
Bristol City 0 - 1 West Ham United
Upangaji wa draw kwa ajili ya hatua ya tano utafanyika hapo kesho jumatatu.
0 comments:
Post a Comment