London,England.
Ligi kuu ya England maarufu kama Epl leo imeendelea kutimua vumbi lake ambapo imeshuhudiwa mvua kubwa ya magoli ikinyesha.
Katika mchezo uliopigwa huko Liberty Stadium wenyeji Swansea City wamekubali kichapo cha magoli 5-0 toka kwa Chelsea.(Wafungaji Costa 2,Oscar 2 na Schurrle 1)
Huko White hart lane wenyeji Spurs waliitandika bila huruma klabu ya Sunderland kwa jumla ya goli 2-1.(Wafungaji Vertoghen,Eriksen-Larsson)
Huko Loftus road magoli ya kiungo Marouane Ferraini na kinda James Wilson yalitosha kuipa Manchester United ushindi ugenini dhidi ya klabu ya Queens Park Rangers.
Huko Villa Park wenyeji Aston Villa wameshindwa kuuzima muziki wa vijana wa Liverpool baada ya kukubali kichapo cha goli 2-0.(Wafungaji Borrin,Lambert)
Huko Saint James Park vijana walio katika kasi ya ajabu wa Southampton leo wameitambia klabu ya Newcastle United baada ya kuibanjua kwa jumla ya magoli 2-1.(Wafungaji Goaufran-Aljero Elia)
Vijana wa Burney walikubali kichapo cha goli 3-2 nyumbani toka kwa wageni Crystal Palace waliochini ya Alan Pardew.(Wafungaji Ben Mee,Ings-Puncheoun,Gayle 2)
Kesho jumapili
Manchester City v Arsenal (1:00 usiku)
0 comments:
Post a Comment