728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, January 16, 2015

    KIJUE KINACHOILETA ARSENAL TANZANIA

    Ujumbe wa Klabu ya Arsenal
    ya England unatarajiwa kuwasili nchini Jumapili hii kuhusu masuala ya soka pamoja na kuwekeza nchini.
    Ofisa Biashara Mkuu wa Arsenal,Venkatesham amesema wameichagua Tanzania kwa wana mashabiki wengi na kwa kushirikiana na taasisi za Tanzania,watakuwa karibu zaidi na mashabiki wao
    kuliko ilivyokuwa awali.

    “Katika bara lenye nchi zaidi ya 50,tumechagua kuzuru Tanzania kimkakati kwa sababu tunaiamini nchi hii.
    Arsenal ina mamilioni ya Watanzania ambao ni mashabiki waaminifu na wenye mapenzi makubwa nayo.”
    Alisema katika ziara yao hiyo ya wiki moja nchini Tanzania, pia watajadili fursa za ushirikiano na wafanyabiashara kadhaa wakubwa nchini Tanzania katika soka.
    Huu utakuwa ujumbe wa kwanza wa Arsenal kutua Tanzania, ambao klabu hii
    kubwa ya Uingereza inataka kujenga ushirika mkubwa katika maeneo ya masoko na chapa zake, ili kutanua
    mafanikio yaliyofikiwa kwenye nchi nyingine za Afrika kama Kenya, Uganda
    na Nigeria.
    Washika Bunduki hao wa London wanataka kutoa fursa kwa benki za Tanzania pamoja na kampuni za simu na taasisi nyingine kupata rasilimali zihusianazo na Arsenal, kama vile bidhaa
    zilizosainiwa kwa majina ya wachezaji,tiketi za mechi.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    1 comments:

    Item Reviewed: KIJUE KINACHOILETA ARSENAL TANZANIA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top