Angelo Henriquez:Kocha mkuu wa klabu ya Dinamo Zagreb ya Croatia Zoran Mamic ametangaza kuwa klabu yake imekamilisha usajili wa mshambuliaji kinda wa klabu ya Manchester United raia wa Chile Angelo Henriquez (19) kwa mamilioni ya Euro.
Henriques ambaye kabla ya uhamisho huo wa kudumu alikuwa akiichezea Zagreb kwa mkopo na kufanikiwa kuifungia jumla ya magoli 15 katika michezo 18 ya ligi ya Croatia msimu huu.
Manchester United ilimsajili Angelo mwaka 2012 toka klabu ya Universidad de Chile kwa ada ya£4m.
Darren Fletcher:Klabu ya Westbrom Wich Albion
West brom inataka kumsajili kiungo huyo ili kwenda kuongeza nguvu baada ya kiungo wake Youssuf Mulumbu kuwa katika majukumu ya kuitumikia timu yake ya Drc Congo katika michuano ya AFCON inayotarajiwa kuanza hivi karibuni huko Equatorial Guinea.
Fletcher ni kati ya nyota wa Manchester United wanaohaha kupata nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza kwani katika msimu huu amebahatika kuanza jumla ya michezo mitatu tu chini ya kocha Louis Van Gaal.
Fletcher amekuwa Manchester United kwa miaka 12 sasa huku akifanikiwa kutwaa jumla ya mataji matano ya ligi kuu na moja la ligi ya mabingwa Ulaya.
0 comments:
Post a Comment