KOCHA Mkuu wa Taifa Stars, Mart Nooij, ametaja kikosi chenye majina ya wachezaji 26 ambacho kinatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Rwanda mnamo Januari 22, mwaka huu kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
Kikosi kamili kilichoitwa ni; makipa, Aishi Manula (Azam), Benedict Tinoco (Kagera Sugar) na Peter Manyika (Simba).
Mabeki, Miraji Adam, Andrew Vincent na Salim Mbonde (wote Mtibwa Sugar), Gadiel Michael (Azam FC), Joram Mgeveke na Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ (wote Simba), Edward Charles (Yanga) na Emmanuel Semwanda wa African Lyon.
Viungo ni Salum Telela, Hassan Dilunga na Said Juma Makapu (wote Yanga), Said Ndemla na Hassan Banda (wote Simba), Hussein Moshi (Geita SC), Omary Nyenje (Ndanda), Shiza Ramadhani (Mtibwa), Adam Paulo na Alfred Juma wanaotokea Bulyankulu SC.
Washambuliaji ni Rashid Mandawa na Atupele Green (wote Kagera Sugar), Simon Msuva (Yanga), Kelvin Friday (Azam) na Aboubakar Ally (White Bird).
0 comments:
Post a Comment