Kocha wa klabu ya daraja la pili ya Cambridge United Richard Money amewaonya nyota wake kutojaribu kubadilishana jezi na nyota wa klabu ya Manchester United.
Money ametoa onyo hilo kuelekea mchezo wa leo wa raundi ya nne wa kombe la FA dhidi ya klabu ya Manchester United utakaopigwa katika dimba la Abbey.
Money amesema mchezo wa leo ni baina ya walio nacho (Manchester United) na wasio nacho (Cambridge United)
"Mchezaji yoyote wa Cambridge atakaye badilishana jezi na mchezaji wa Manchester United baada ya mchezo ni lazima aende kwenye duka la klabu na kununua jezi nyingine.
"Na atakaye badilishana jezi wakati wa mapumziko ajue kabisa kuwa atacheza kipindi cha pili akiwa kifua wazi"Alimaliza Money
Jezi moja katika duka la klabu ya Cambridge inauzwa kwa £39.99
0 comments:
Post a Comment