London,England.
Chama cha soka cha England FA kimemfungia michezo mitatu mshambuliaji hatari wa klabu ya Chelsea Diego Costa 26 baada ya kumkuta na hatia ya kumkanyaga kwa makusudi kiungo wa Liverpool Emre Can.
Costa alifanya kosa hilo jumanne ya wiki hii katika mchezo wa nusu fainali wa kombe la Capital One.
Michezo atakayokosa Costa ni pamoja na mchezo wa kesho dhidi ya Manchester City,Everton kisha Aston Villa.
Wakati huo huo klabu ya Chelsea imeripotiwa kuwa mbioni kumfanyia vipimo vya afya siku ya jumamosi nyota Juan Cuadrado 26 kabla ya kumsajili rasmi kwa ada ya £26.8m.
0 comments:
Post a Comment