Kocha Mkuu wa timu ya Taifa Tanzania Taifa Stars’, Mart Nooij amezitaja Senegal
na Ivory Coast kuwa ni timu zenye nafasi kubwa ya kutwaa taji la Mataifa Afrika
(Afcon), zilizoanza kutimua vumbi juzi,Equatorial Guinea.
na Ivory Coast kuwa ni timu zenye nafasi kubwa ya kutwaa taji la Mataifa Afrika
(Afcon), zilizoanza kutimua vumbi juzi,Equatorial Guinea.
Nooij alisema
anaamini fainali za mwaka huu zitakuwa na ushindani mkubwa,lakini Senegal na Ivory Coast zina nafasi kubwa ya kubeba taji hilo.
Nooij alisema Senegal inaundwa na wachezaji wengi vijana wenye vipaji ambao tayari wameshapevuka kisoka ikilinganishwa na nchi nyingine zinazoshiriki mashindano hayo na hiyo ni
faida kwao.
faida kwao.
“Nimekitazama kikosi cha Senegal,nadhani watafanya vizuri mwaka huu na wanaweza kutwaa ubingwa.
"Wana kikosi chenye wachezaji ambao wana kiu ya mafanikio. Nimekuwa nikiwafuatilia wengi tangu nilipokuwa mmoja wa wataalamu wa ufundi wa Chama cha Soka Uholanzi,” alisema Nooij.
Kuhusu Ivory Coast, Nooij alisema kuwapo wa mastaa wengi wanaotamba kwenye ligi mbalimbali barani Ulaya kunaweza kuwa chachu ya wao kutamba kwenye mashindano ya mwaka huu.
“Ivory Coast nayo naipa nafasi ya kutwaa taji mwaka huu kutokana na kikosi chao kujaza wachezaji wengi wenye uzoefu.
Iwapo watakuwa kwenye ubora wao,ninaamini kabisa kuwa hakutakuwa na timu ya kuwazuia,” aliongeza Nooij.
Mechi za awali katika Fainali za Mataifa ya Afrika zilianza kwa wenyeji Equatorial Guinea kulazimishwa sare 1-1 Kongo,wakati Gabon ikiichapa Burkina Faso 2-0.Ghana itachuana na Senegal wakati Algeria itakutana na Afrika Kusini.
0 comments:
Post a Comment