728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, January 17, 2015

    HABARI ZOTE MPYA ZA USAJILI ZIKO HAPA

    Song:Kocha wa klabu ya Westham Sam Allardyce amesema klabu yake tayari imeshaandaa dau la £11.5m kwa ajili ya kumsajili moja kwa moja kiungo wa klabu ya Barcelona aliyeko klabuni hapo Mcameroon Alex Song (27).Mbali ya Westham vilabu vingine vinavyomtaka Song ni pamoja na Liverpool na Manchester United.

    Dijk:Mlinzi wa klabu ya Celtic Muholanzi Virgil van Dijk ameiambia klabu ya Arsenal kuwa ifanye haraka kuja kumsajili ili atimize ndoto ya kucheza ligi kuu ya England.

    Clyne:Klabu ya Manchester United imeripotiwa kukata tamaa ya kumsajili kiungo wa As Roma Kevin Strootman mwezi huu na badala yake inaelekeza nguvu zake kwa mlinzi wa kulia wa klabu ya Southampton Nathaniel Clyne (23).

    Zaza:Klabu ya Tottenham imeingia katika mbio za kumuwania mshambuliaji wa klabu ya Sassuolo Simone Zaza.Hata hivyo Tottenham itakabiriwa na ugumu katika usajili huo kutokana na mchezaji huo kumilikiwa pia na klabu ya Juventus.

    Salah:Klabu ya As Roma imeripotiwa kuandaa ofa ya £11.5m kwa ajili ya winga wa klabu ya Chelsea Mohammed Salah kiasi ambacho ni pungufu ya kile cha £13m kilichopo katika mkataba wa nyota huyo mzaliwa wa Misri.

    Arbeloa:Kocha wa Chelsea Jose Mourinho anafikiria tena kumsajili mlinzi wake wa zamani katika klabu ya Real Madrid Alvaro Arbeloa (32).Arbeloa amekosa nafasi katika kikosi cha kwanza cha kocha Carlo Ancellotti.

    Fiorentina:Klabu ya Fiorentina imeripotiwa kuingia katika mbio za kuiwania saini ya kiungo wa Southampton Mkenya Victor Wanyama ambaye pia anawaniwa na vilabu vya Manchester United na Inter Milan.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: HABARI ZOTE MPYA ZA USAJILI ZIKO HAPA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top