Ebebiyin.
Michuano ya AFCON iliendelea tena jana jumapili kwa michezo miwili ya kundi B iliyopigwa katika dimba la Nuevo Estadio de EbebiyÃn.
Katika mchezo wa mchezo wa mapema Zambia na Congo DRC ziligawana pointi baada ya kutoka sare ya goli 1-1.Goli la Zambia lilifungwa na Given Singuluma kabla ya Yennick kuisawazishia Congo.
Katika mchezo wa pili sare pia iliendelea kutawala baada ya Tunisia na Cape Verde kufungana goli 1-1.Goli la Tunisia lilifungwa na Mohamed Manser huku Cape Verde wakisawazisha kwa mkwaju wa penati ulifungwa na Almeida Heldon.
Leo jumatatu kutakuwa na mechi mbili za kundi C ambapo Ghana watacheza na Senegal huku Algeria wakivaana baadae na Afrika ya Kusini.
Mechi ambazo zote zitapigwa katika dimba la Estadio de Mongomo,Mjini Mongomo .
0 comments:
Post a Comment