London,England.
Rasmi leo klabu ya Arsenal imekamilisha usajili wa mlinzi Mbrazil Gabriel Paulista 24 toka klabu ya Villarreal kwa ada ya £11.5m.
Gabriel aliyeanzia soka katika klabu ya Vitorio ametua Arsenal baada ya kupata kibari cha kufanyia kazi nchini England.
Katika kukamilisha usajili huo Arsenal imelazimika kumtoa kwa mkopo nyota wake Joel Campbell ili kumpata Paulista ambaye sifa yake kubwa ni kumudu nafasi nyingi za sehemu ya ulinzi.
Baada ya kukamilisha usajili wake Paulista ameahidi kufanya makubwa na klabu ya Arsenal huku akisisitiza kuwa ndoto yake ya kuchezea moja kati ya vilabu vikubwa duniani imetimia.
0 comments:
Post a Comment