Alcacer:Klabu ya Valencia inajipanga kumpa mkataba mpya nyota wake Paco Alcacer (21) utakaoisha mwaka 2020 huku ikiweka kipengere cha kumuuza kwa €70m.
Stoke City:Klabu ya Stoke City iko mbioni kukamilisha usajili wa mkopo wa makinda wawili wa klabu ya Barcelona Adama Traore na Sandro.
Grosskreutz:Klabu ya Arsenal imeripotiwa kuisaka saini ya kiungo wa klabu ya Borrussia Dortmund Kevin Grosskreutz kwa ada ya £3.7m.
Akpom:Klabu ya Liverpool imeripotiwa kuwa miongoni mwa vilabu vinavyoiwania saini ya mshambuliaji kinda wa klabu ya Arsenal Chuba Akpom (19) anaye maliza mkataba wake mwishoni mwa msimu huu.
Milner:Klabu ya Liverpool ina matumaini ya kumsajili kwa uhamisho huru mwishoni mwa msimu nyota wa klabu ya Manchester City James Milner ambaye amegoma kuongeza mkataba mpya wa kuendelea kubaki klabuni hapo.
Fletcher:Klabu ya Manchester United imeripotiwa kukubali kumuachia kiungo wake Darren Fletcher 30 anayewindwa na vilabu vya Celtic,Westham,Valencia na West Brom.
Laporte:Klabu ya Real Madrid ineripotiwa kuanza mbio za kutaka kumsajili mlinzi wa klabu ya Atletico Bilbao Aymeric Laporte (21) lakini italazimika kutoa kiasi cha €42m kinachotakiwa na Bilbao.
Taarabt:Klabu ya Ac Milan iko katika mazungumzo na klabu ya QPR kwa ajili ya kumsajili winga Mmoroco Adel Taarabt.
0 comments:
Post a Comment