Malabo,Guinea.
Shirikisho la kandanda barani Afrika CAF limesema litaupitia upya utaratibu wa kumpata mshindi kwa njia ya bahati nasibu baada ya timu kuwa sawa katika hatua ya makundi.
Hapo juzi Guinea iliingia robo fainali kwa ushindi wa mezani baada ya kubahatika kwenye bahati nasibu hiyo huku Mali ikifungasha virago baada ya timu zote mbili kumaliza mechi za makundi zikiwa zote zina point tatu na magoli matatu.
Hadi mechi za kundi D katika hatua za makundi zinamalizika hapo juzi, ni Ivory Coast pekee ndio iliyoingia robo fainali baada
ya kuifunga Cameroon.
Utarabu wa kumpata mshindi kwa njia ya bahati nasibu umekosolewa na wapenzi wa
soko kwamba hautendi haki.
Mkurugenzi wa habari wa shirikisho la soka Afrika Junior Binyam amesema pamoja na kwamba walipaswa kusimamia kanuni za mashindano hayo lakini anadhani ipo haja ya kuboresha utaratibu wa kumpata mshindi pindi tukio kama hilo linapotokea.
Amesema sio haki timu kurudi nyumbani kama ilivyofanyika kwa Mali.
0 comments:
Post a Comment