728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, January 23, 2015

    MPYA ZA USAJILI JIONI HII HIZI HAPA

    Alves:Kocha wa klabu ya Manchester United Louis Van Gaal ameripotiwa kutaka kumtumia mlinda mlango Victor Valdes ili kumshawishi mchezaji mwenzie katika klabu ya Barcelona Dani Alves 31 ili atue Old Trafford pindi mkataba wake utakapokwisha mwezi juni.

    M'Villa:Klabu ya Inter Milan imeamua  kuvunja mkataba wa mkopo wa kiungo wa Rubin Kazan Yann M'Villa baada ya kutoridhishwa na kiwango chake tangu atue klabuni hapo mwezi agosti.

    Rodriguez:Klabu ya Liverpool imejipanga kufanya usajili wa kushitukiza wa mshambuliaji aliyekuwa majeruhi wa klabu ya Southampton Jay Rodriguez.Rodriguez pia anawindwa na klabu ya Tottenham Hot Spurs.

    Nainggolan:Klabu ya Arsean imeambiwa iandae dau la £26m kama kweli inataka kumsajili kiungo wa klabu ya As Roma Radja Nainggolan 26.Vilabu vingine vinavyohusishwa kumtaka kiungo huyo ni Manchester United,Chelsea na Liverpool.

    Szczesny:Hatima ya mlinda mlango Wojciech  Czeszney katika klabu ya Arsenal imeendelea kuchukua sura mpya kila siku baada ya taarifa za hivi punde kudai kuwa Arsenal imeanza kusaka mlinda mlango mpya atayekuja na kuwa chaguo la kwanza.Walinda mlango wanaotajwa ni Neto (Fiorentina) Peter Cech (Chelsea)

    Souare:Taarifa toka ndani ya klabu ya Lille zinasema kuwa mlinzi wake wa kushoto Pape Souare anakaribia kutua katika klabu ya Crystal Palace kwa dau la €4.5m kwa mkataba wa miaka mitatu na nusu.

    Pato:Kutoka Brazil habari zinasema klabu ya Corinthians inataka kumtoa kwa mkopo mshambuliaji wake Alexandre Pato 25 katika klabu ya QPR.Kwa sasa Pato yuko kwa mkopo katika klabu ya Sao Paulo na amefanikiwa kufunga jumla ya mabao 12 msimu huu.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MPYA ZA USAJILI JIONI HII HIZI HAPA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top