728x90 AdSpace

Tuesday, January 13, 2015

KOCHA JULIO ADUNDWA MUSOMA

Musoma,Tanzania.

Kocha wa Mwadui FC, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amekumbana na balaa mjini Musoma.

Julio amepigwa jiwe na kujeruhiwa wakati timu yake ya Mwadui FC ikicheza mechi ya Ligi Daraja la Kwanza dhidi ya Polisi Mara.

Mechi hiyo ilichezwa wikiendi mjini Musoma na kumalizika kwa sare ya mabao 2-2.

Hali hiyo ilisababisha mashabiki wa Polisi kuanza kuwashambulia Julio na wachezaji wake ambao baadhi walijeruhiwa.

“Kweli nimepigwa jiwe la mgongoni na sasa siko vizuri. Nimeshindwa hata kwenda mazoezini.

“Hakika hawakututendea haki na
askari polisi hawakuwa na msaada,” alisema Julio.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: KOCHA JULIO ADUNDWA MUSOMA Rating: 5 Reviewed By: Unknown