Dragovic:Habari kutoka England zinadai kuwa klabu ya Manchester United imekubali kumsajili mlinzi wa kati wa klabu ya Dinamo Kiev Aleksandar Dragovic kwa ada ya £15m.
Konoplyanka:Klabu ya Everton inajipanga kumsajili kwa bei chee winga wa klabu ya Dnipro ya Ukraine Yevhen Konoplyanka aliye mbioni kumaliza mkataba wake ili kuja kuchukua nafasi ya Kevin Mirallas aliyegomea mkataba mpya Goodson Park.
McManaman:Klabu ya West Brom bado inaendelea kunyatia winga wa Klabu ya Wigan Callum McManaman (23) baada ya kuripotiwa kuongeza dau mpaka £4.5m ili kumnasa mapema winga huyo mwenye chenga za maudhi.
Mancini:Kocha wa Inter Milan Roberto Mancini ametajwa kuwa chaguo la katika klabu ya PSG ili kuchukua nafasi ya kocha Laurent Blanc anayetarajiwa kutimka klabuni hapo mwishoni mwa msimu.
Toure:Kiungo wa klabu ya Manchester City Yaya Toure (31) amekaririwa akisema kuwa anafikiria kupunguza kiwango cha mshahara wake ili aweze kujiunga na klabu ya Inter Milan inayofundishwa na kocha wake wa zamani Roberto Mancini.
Sterling:Baada ya kuripotiwa kugomea mkataba mpya aliopewa na klabu yake ya Liverpool,winga Raheem Sterling amegeuka dili kwa vilabu vya Chelsea na Real Madrid kwani vimedaiwa kuanza kujisogeza zaidi na nyota huyo mwenye kasi ili viinase saini yake wakati wa majira ya joto.
Destro:Baada ya kufanikiwa kumpata mlinzi Gabriel Paulista klabu ya Arsenal imeripotiwa kuwa katika mawindo ya kumnasa mshambuliaji wa As Roma Mattia Destro (23) kwa mkopo kabla ya kumsajili moja kwa moja mwisho wa msimu kwa £15m.
0 comments:
Post a Comment