Icardi akiwajibika dimbani |
Dirk Kuyt:Vilabu vya Ac Milan,Westham United,Lyon na Valencia vimeripotiwa kuisaka saini ya mshambuliaji wa klabu ya Fenerbahce ya Uturuki Dirk Kuyt 34 anayemaliza mkataba mwezi juni.
Mauro Icardi:Vilabu vya Liverpool na
Chelsea kwa pamoja vimeripotiwa kuanza kumfukuzia mshambuliaji kinda wa Inter Milan Mauro Icardi 21 mwenye thamani ya £26m.Icardi ameifungia Inter magoli 10 katika michezo 18.
Lukas:Kiungo wa klabu ya Liverpool Mbrazil Lukas Leiva ameripotiwa kuichoka klabu hiyo na anafanya kila awezalo atimke januari hii na kutua Inter Milan ya Italia.
Bishop:Klabu ya Liverpool imeripotiwa kuwa mbele kabisa katika mbio za kumnasa kiungo kinda wa klabu ya Ipswich town Teddy Bishop 18.
Xavi:Kiungo wa klabu ya Barcelona ya Hispania Xavi Hernandez amewataka viungo wenzie wa Kispania Santi Cazorla na David Silva kuja kucheza katika klabu hivyo kwa kuwa wana sifa zote zinazotakiwa.
0 comments:
Post a Comment