Paul Manjale,Dar Es Salaam.
STAA wa Manchester United,Zlatan Ibrahimovic ametanjwa kuingia kwenye kinyang'anyiro cha kumsaka mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa msimu wa ligi kuu nchini England maarufu kama PFA Player of the Year award.
Wengine waliotanjwa kuingia kwenye kinyang'anyiro ni pamoja na Alexis Sanchez wa Arsenal,mshindi wa mwaka juzi wa tuzo hiyo Eden Hazard wa Chelsea na N’Golo Kante wa Chelsea pia.
Wengine ni staa wa Everton,Romelu Lukaku pamoja na Harry Kane wa Tottenham
Hotspur ambapo pia wametajwa kwenye kinyang'anyiro cha kumsaka mchezaji bora wa mwaka kijana (Chipukizi)
Mlinzi wa Middlesbrough, Michael Keane ni mmoja kati ya wachezaji sita ametanjwa kuingia kwenye kinyang'anyiro cha kumsaka mchezaji bora wa mwaka kijana (Chipukizi).
Wengine ni Romelu Lukaku wa Everton,Harry Kane wa Tottenham Hotspur.Leroy Sane wa Manchester City, Jordan Pickford wa Sunderland na Deli Alli wa Tottenham Hotspurs.Washindi watatangazwa Jumapili ya Aprili 23.
Mchezaji bora wa mwaka kwa wachezaji wa kiume (Men’s PFA Players’ Player of the Year)
Eden Hazard (Chelsea), Zlatan Ibrahimovic (Man Utd), Harry Kane (Tottenham),
N’Golo Kanté (Chelsea), Romelu Lukaku (Everton), Alexis Sánchez (Arsenal)
Mchezaji bora wa mwaka kwa wachezaji vijana (Men’s PFA Young Player of the Year)
Harry Kane (Tottenham), Dele Alli (Tottenham), Romelu Lukaku (Everton),
Michael Keane (Burnley), Jordan Pickford (Sunderland), Leroy Sané (Manchester City).
Mchezaji bora wa mwaka kwa wachezaji wa kike (Women’s PFA Players’ Player of the Year)
Lucy Bronze (Manchester City), Karen Carney (Chelsea), Jane Ross (Manchester City), Jill Scott (Manchester City), Caroline Weir (Liverpool), Ellen White
(Birmingham)
Mchezaji bora wa mwaka kwa wachezaji vijana (Women’s PFA Young Player of the Year)
Millie Bright (Chelsea), Jess Carter (Birmingham), Nikita Parris (Manchester City), Georgia Stanway (Manchester City), Keira Walsh (Manchester City), Caroline Weir (Liverpool)
0 comments:
Post a Comment