Mbeya,Tanzania.
VILABU vya Mbeya City na African Lyon vimeshindwa kutambiana baada ya jioni ya leo kufungana bao 1-1 kwenye mchezo mkali wa wa ligi kuu bara uliochezwa kwenye uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.
Wenyeji Mbeya City ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 42 ya kipindi cha kwanza kupitia kwa kiungo wake mahiri, Raphael Daudi.Bao hilo lilidumu mpaka mapumziko.
Kipindi cha pili African Lyon walikuja juu na kufanikiwa kupata bao la kusawazisha katika dakika ya 57 kupitia kwa Thomas Morris aliyefunga kwa mkwaju wa penati na kufanya mchezo huo uishe kwa sare ya kufungana bao 1-1.
Aidha katika mchezo huo ilishuhudiwa Mbeya City ikimaliza na wachezaji kumi uwanjani baada ya John Jerome kutolewa nje kwa kadi nyekundu.
Ligi hiyo itaendele Jumamosi kwa michezo minne, Stand United wakiwa wenyeji wa
Mtibwa Sugar ya Morogoro Uwanja wa Kambarage,Shinyanga na Toto Africans
wakiikaribisha Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
Mechi nyingine za Jumamosi, Majimaji ya Songea itaifuata Ruvu Shooting Uwanja wa Mabatini mkoani Pwani -mchezo utakaoanza saa 8.00 mchana wakati JKT Ruvu watakuwa wenyeji wa Azam FC Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga.
Kwa mujibu wa ratiba,Jumapili Mbao watacheza na Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza huku Mwadui wakiwa wenyeji wa Ndanda FC ya Mtwara Uwanja wa Mwadui,Shinyanga.
0 comments:
Post a Comment