Mwandishi Wetu,Dar Es Salaamm.
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetangaza kuikata Klabu ya Kagera Sugar alama tatu pamoja na magoli matatu baada ya kukiuka kanuni za Ligi Kuu ya Vodacom kwa kumchezesha mchezaji ambaye haruhusiwi kucheza.
Akizungumzia hatua hiyo, Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas Mapunda amesema Kagera Sugar ilimchezesha beki wake Mohamed Fakhi akiwa na kadi tatu za njano katika mchezo wa ligi kuu ya dhidi ya Simba kitendo ambacho ni tofauti na kanuni.
Amesema kutokana na kanuni na sheria za ligi kuu, timu ambayo inafanya kitendo hicho inatakiwa kukatwa alama tatu na magoli matatu hivyo na Kagera Sugar imechukuliwa hatua hiyo ambayo itakuwa ni funzo kwa vilabu vingine.
“Kagera walimchezesha Fakhi katika mchezo uliochezwa Aprili, 2 katika uwanja wa kaitaba, Mjini Kagera dhidi ya Simba ni kinyume na kanuni na wanatakiwa kuadhibiwa kwa kunyanganywa alama tatu na magoli matatu,” amesema Mapunda.
Baada ya kukatwa alama sasa Kagera Sugar, Yanga wameshushwa nafasi moja kutoka nafasi ya kwanza hadi ya Pili na Simba Kurudi kileleni kwa ligi Kuu kwa Point 61 huku Yanga ikibaki na pointi 56.
0 comments:
Post a Comment