Valencia, Hispania.
KRC Genk ya Mtanzania, Mbwana Samatta imeshindwa kufanya maajabu ugenini baada ya Alhamis Usiku kushindwa kulianda bao lao la mapema na kujikuta ikikubali kichapo cha mabao 3-2 kutoka kwa wenyeji wao Celta Vigo katika mchezo mkali wa mkondo wa kwanza wa hatua ya robo fainali ya michuano ya Europa Ligi.
Katika mchezo huo uliochezwa huko Balaidos na kushuhudiwa na watanzamaji 18,000 ilishuhudiwa wageni KRC Genk wakiwaweka roho juu wenyeji wao baada ya kupata bao la kuongoza lililofungwa kwa kichwa na Jean-Paul Boetius katika dakika ya 10.
Dakika saba baadae wenyeji Celta Vigo walirekebisha makosa yao na kujipatia mabao mawili ya haraka haraka yaliyofungwa na Pione Sisto pamoja na Iago Aspas kabla ya John Guidetti kuongeza bao la tatu kabla ya mapumziko.
Kiungo mkongwe,Thomas Buffel aliifungia bao la pili KRC Genk na kufanya mchezo uishe kwa matokeo ya wenyeji Celta Vigo kuchomoza na ushindi wa mabao 3-2.Timu hizo zitarudiano wiki ijayo huko Genk na timu itakayokuwa imepata ushindi mkubwa wa jumla itafuzu hatua ya nusu fainali.
0 comments:
Post a Comment