Brussels,Ubelgiji.
Manchester United imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Anderlecht katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa hatua ya robo fainali ya michuano ya kombe la Europa Ligi uliochezwa Alhamis Usiku huko Constant Vanden Stock Stadium jijini Brussels, Ubelgiji.
Henrikh Mkhitaryan alianza kuifungia bao la kuongoza Manchester United katika dakika ya 36 ya mchezo kwa mkwaju wa karibu lakini katika dakika ya 86 ya mchezo makosa ya mlinzi Matteo
Darmian yalitoa nafasi kwa Leander Dendoncker kuifungia Anderlecht bao la kusawazisha kwa kichwa na kufanya mchezo huo uishe kwa sare ya bao 1-1.
Timu hizo zitarudiana tena Aprili 20 mwaka huu huko Old Trafford jijini Manchester.
Latika mchezo mwingine Olympique Lyon ikiwa nyumbani Parc Olympique Lyonnais imelazimika kutoka nyuma na kuifunga Beskitas ya Uturuki mabao 2-1 shukrani kwa mabao ya Corentin Tolisso na Jeremy Morel.Bao la Besiktas limefungwa na Ryan Babel.
Shalke 04 imefungwa mabao 2-0 na Ajax Amseterdam huko Amsterdam Arena shukrani kwa mabao ya Klaassen.
0 comments:
Post a Comment