728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, April 13, 2017

    Arsenal yaamua kumwaga noti za maana kwa Alexis Sanchez


    London,England.

    ARSENAL inajiandaa kumfanya staa wake,Alexis Sanchez kuwa mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa zaidi kwenye historia ya ligi kuu nchini England hii ni baada ya kuripotiwa kumwandalia mkataba mpya wa miaka minne utakaomwezesha raia huyo wa Chile kuvuna mshahara wa Pauni 300,000 kwa wiki.

    Kutoka The Evening Standard habari zinasema Arsenal imekuja na ofa hiyo nono baada ya kushuhudia ofa zake tatu za awali zikipigwa chini na kambi ya Sanchez ambayo imekuwa ikitaka  mteja wao alipwe Pauni 200,000 ndipo asaini mkataba mpya.

    Mesut Ozil kwa sasa ndiye mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa zaidi klabuni Arsenal akivuna mshahara wa Pauni 140,000 kwa wiki.Nafasi ya pili inashikwa na Sanchez anayelipwa mshahara wa sasa wa ni Pauni 130,000 kwa wiki.

    Ikumbukwe Sanchez amebakiza miezi 12 kwenye mkataba wake wa sasa.Hivyo Arsenal imeona dawa pekee ya kuituliza akili ya staa huyo wa zamani wa Udinese ni kumpa mkataba mnono wenye maslahi mazuri zaidi.

    Kwa sasa Paul Pogba wa Manchester United ndiye mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa zaidi ligi kuu England.Analipwa 290,000 kwa wiki.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Arsenal yaamua kumwaga noti za maana kwa Alexis Sanchez Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top