728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, April 13, 2017

    Kiboko ya Barcelona alamba dili jipya Juventus



    Torino,Italia.

    ULIUTAZAMA vyema mchezo wa juzi Jumanne wa robo fainali ya kwanza ya ligi ya mabingwa Ulaya kati ya Juventus na Barcelona?Unayakumbuka matokeo yake?Ndio Barcelona ilichapwa mabao 3-0.Kuna jamaa alifunga mabao mawili siku hiyo.Bhasi yule jamaa aliyefunga mabao hayo mawili anaitwa Paulo Dybala.

    Ishu iko hivi staa huyo wa zamani wa Palermo amesaini kandarasi mpya ya miaka mitano ya kuendelea kusalia Juventus mpaka Juni 30, 2022.

    Kandarasi hiyo mpya haijamuacha hivi hivi Dybala,23, bali pia imemuwezesha staa huyo kutoka Argentina kuvuna kitita cha €135,000 kama mshahara wa wiki na kuwa mchezaji wa pili anayelipwa mkwanja mrefu zaidi Seria A nyuma ya Gonzalo Higuain.

                        

    Dybala alijiunga na Juventus mwaka 2015 akitokea Palermo kwa ada ya awali ya Euro Milioni 32.Mpaka sasa Dybala ameifungia Juventus mabao 27 katika michezo 58.Katika msimu wake wa kwanza Dybala aliiwezesha Juventus kutwaa ubingwa wa Seria A na ubingwa wa Coppa Italia.




    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Kiboko ya Barcelona alamba dili jipya Juventus Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top