728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, April 13, 2017

    Baada ya kusimamishwa , Abdi Banda akwea pipa kwenda South Africa



    Mwandishi Wetu,Dar Es Salaam.

    Baada ya Banda kusimamishwa kucheza ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara Kwa kosa la kumpiga ngumi kiungo wa Kagera sugar George Kavilla wakati akiwa hana Mpira. Leo  Banda kukwea pipa kuelekea Afrika kusini Kwa Ajili ya Mazungumzo ya mkataba na moja ya timu huko Afrika kusini. 

    Habari za kuaminika Banda alikuwa Dar Tangu Jumamosi akifanya utaratibu wa safari yake 

    " Ndio naenda Afrika kusini Kwenye Mazungumzo na timu moja huko na sitakaa muda mrefu maana naenda kwa Mazungumzo kuhusu mkataba na si kufanya Majaribio Sizani kama hata wiki itaisha"
    Alisema Abdi Banda 

    Mkataba wa Banda na Simba unaisha mwisho wa msimu Banda yuko huru kufanya mazungumzo na timu yoyote lakini Simba walimpa mkataba mpya ili ausome na akikubaliana nao ausaini lakini wakala wa Bandaa alisitisha kusaini mkataba mpya mpaka mwisho wa msimu. 

    Wakati Banda akiondoka leo kwenda Afrika kusini kamati ya nidhamu ya Tff itakaa leo saa tisa katika ukumbi uliopo uwanja wa uhuru  kupitia shauri lake la kusimamishwa na kamati ya mashindano na Usimamizi (kamati ya masaa 72) kucheza mechi za ligi kuu kwa kosa la kumpiga ngumu mchezaji wa kagera sugar. 

    Wakati Banda ikiondoka amesema ana Baraka zote kutoka kwa Uongozi wa timu ya Simba  Alisema ''Nimewaaga viongozi wangu na wanafahamu juu ya Hii safari, haya ni maisha yangu kupitia Soka hivyo natakiwa niangalie kotekote,   nimekosa Mechi dhidi ya Mbao nitakosa pia mechi dhidi Toto baada ya hapo nitakuwa nimerudi ila itategemea na maamuzi ya kamati " 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Baada ya kusimamishwa , Abdi Banda akwea pipa kwenda South Africa Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top