728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, April 06, 2017

    Wachezaji wa Yanga watishia kugoma kisa Mshahara


    Faridi Miraji , Dar es salaam.                          


    Wachezaji wa Yanga wametishia kugomewa mechi ya kimataifa dhidi ya MC Alger itakayochezwa Jumamosi  Uwanja wa taifa.  Kulikuwa na hali ya sintofahamu ndani Yanga leo wachezaji wa Yanga Wamepeleka malalamiko yao Kwa meneja wakilalamikia mshahara  Wao kuchelewa na malimbikizo ya  nyuma ambayo aliahidiwa Tangu mechi dhidi ya Simba. Wachezaji hao Wamekaa kikao cha pamoja na kuridhia Kwa kauli moja kama hawatalipwa fedha zao kabla ya Jumamosi hawataingia uwanjani.  Mwanzoni kulikuwa na mpango wa kugomea hadi mazoezi ila walikubaliana kwenda kwenye mazoezi mpaka Ijumaa Jioni. 
                     
    Baada ya kusikia mwachezaji kutishia kugoma  Katibu wa Yanga Boniface Mkwasa amesema "Nimepata dharula nipo nje kidogo ya Dar, nipo Morogoro msibani kwa kaka yangu. Kiukweli kama wataamua kugoma kisa mshahara wa mwezi mmoja na malimbikizo ya deni lao la nyuma binafsi watanisikitisha sana ukizingatia ni mchezo mgumu ambao pia ni mhimu kwao kujitangaza, sitawaelewa kabisa. Hali inaeleweka mwenyekiti ambaye alikuwa mdhamini alipata matatizo na hadi leo ofisini hajafika Sasa hapo tutafanyaje??

    Tumeshaandaa mchakato wa kufanya harambee ya kuichangia klabu yetu pia kuna hela tunasubiri ambazo zimeshikiliwa na bodi ya ligi, hizo pesa zikitoka basi tumekusudia kuwalipa haraka. Swala la kukopa lina utaratibu wake mfano kuna riba na kuweka mali bond, hatutaki kufika huko maana tunajua kuna hela zetu ambazo zitaingia, hela wanazotudai ni milioni 400 ni pesa nyingi ambazo hatuna jinsi lazima wasubiri tu. leo ni tarehe 5 (jana)  kuna mashirika huchelewesha mishahara hata kwa miezi miwili lakini wafanyakazi huendelea kufanya kazi. Pia tumejaribu kumtaarifu mwenyekiti hali halisi ya sasa kwenye timu "

    Hii si Mara ya kwanza ya Yanga kugoma mwaka jana mwezi Desemba,19 pia waligoma kufanya mazoezi Kwa sababu ya kucheleweshewa mshahara  wa November .  Hili ni pigo kubwa kwa vilabu vyetu rasilimali watu walizonazo wanatakiwa kuzitumia vizuri ili kutoa huu utegemezi unaotishia maendeleo ya klabu.  Ni udhaifu wa hali ya juu klabu iliyoazishwa mwaka 1935 na inakadiliwa kuwa na wanachama na mashabiki taklibani milion 7-10 Tanzania nzima  inategemea mfadhili mmoja.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Wachezaji wa Yanga watishia kugoma kisa Mshahara Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top