728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, April 06, 2017

    Bila Ronaldo,Bale Real Madrid bado moto tu,yashinda 4-2 ugenini


    Leganes,Hispania.

    IKICHEZA bila ya nyota wake wawili,Cristiano Ronaldo na Gareth Bale waliopumzishwa kwa sababu mbalimbali,Real Madrid Jumatano usiku imepata ushindi mnono wa mabao 4-2 ugenini Butarque dhidi ya wenyeji wao Leganes katika muendelezo wa michezo ya ligi ya La Liga.

    Alvaro Morata ndiye aliyekuwa nyota wa Real Madrid kwenye mchezo huo baada ya kufunga mabao mawili katika dakika za 18 na 23.Bao la tatu limefungwa na James Rodriguez dakika ya 15 huku bao la nne likifungwa dakika ya 48 na beki Martin Mantovani aliyejifunga akiwa katika harakati za kuokoa hatari langoni mwake.

    Mabao ya wenyeji Leganes yamefungwa na Gabriel Appelt Pires dakika ya 32 pamoja na Luciano dakika ya 34 ya kipindi cha kwanza.Mabao hayo yameifanya Real Madrid ifikishe pointi 71 na kurejea nafasi ya kwanza La Liga, pointi mbili mbele ya Barcelona yenye pointi 69.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Bila Ronaldo,Bale Real Madrid bado moto tu,yashinda 4-2 ugenini Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top