728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, April 06, 2017

    Alichokisema Mkwasa baada ya wachezaji Yanga SC kudaiwa kutaka kugoma


    Paul Manjale,Dar Es Salaam.

    KATIBU MKUU wa Yanga SC,Charles Mkwasa amewataka wachezaji wa klabu hiyo kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kigumu cha mdororo wa kiuchumi kinachoikumba miamba hiyo ya soka nchini.

    Mkwasa ametoa kauli hiyo baada ya kuwepo kwa taarifa kuwa wachezaji wa klabu hiyo wanataka kugomea mchezo wao wa Jumamosi wa Jumamosi wa kombe la shirikisho Afrika dhidi ya MC Alger kwa madai ya mishahara yao.

    Akiongea na kituo kimoja cha redio cha jijini hapa,Mkwasa ambaye kwa sasa yuko mkoani Morogoro alikokwenda kuhudhuria msiba wa kaka yake amekiri kweli Yanga SC inadaiwa mishahara na wachezaji wake lakini amesema kama kweli wachezaji hao wataamua kugoma kwa madai ya mshahara wa mwezi mmoja basi watakuwa wanakosea sana.

    Mkwasa ameongeza kuwa uongozi wa Yanga SC unafahamu kuwepo kwa deni hilo lakini amewataka wachezaji kuendelea na maandalizi ya mchezo wao wa Jumamosi katika kipindi hiki ambapo uongozi unapambana kwa kila hali kupata fedha ili kuwalipa mishahara na madai yao mengine yanayofikia Milioni 400.

    "Ni kweli wachezaji wanadai mishahara yao pamoja na malimbikizo yao mengine ya nyuma.Uongozi unapambana kuhakikisha unapata fedha kwa ajili ya kulipa deni hilo.Tutalipa muda si mrefu,tayari tumeshaongea na wanachama pamoja na wadau mbalimbali ili watusaidie.Pia tumeshafanya mawasiliano na bodi ya ligi ambayo tunaidai malimbikizo ya fedha za haki za matangazo ya televisheni.Alisema Mkwasa.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Alichokisema Mkwasa baada ya wachezaji Yanga SC kudaiwa kutaka kugoma Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top