728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, April 06, 2017

    Simba Sc kumkosa Mkude mechi na Mbao Fc Jumatatu


    Faridi Miraji , Dar es salaam.                               

    Simba Ambayo imetoka kujeruhiwa na  Kagera sugar  Kwa kufungwa magoli mawili Kwa moja Katika mchezo huo walimkosa beki wa kimataifa wa Congo,Javier Besela Bukungu aliyekuwa anatumikia adhabu ya kadi nyekundu aliyoipata kwenye mechi dhidi ya Yanga,  Bukungu alikosa mechi mbili dhidi ya Mbeya City na Kagera Sugar.   Jumatatu ya April 10 Simba watamkosa Nahodha Wao Jonas Mkude Kwa kuwa na kadi tatu za njano, Mkude alipewa kadi ya njano kwenye Pambano dhidi ya Kagera na sasa Atakosa mchezo dhidi ya Mbao na ataungana na timu kwenye mechi dhidi ya Toto African ya Mwanza pia.

    Kutokana na kukosekana Kwa nahodha Jonas  Mkude Kikosi cha Simba kinachoweza kuanza. Jumatatu na Mbao ni  Daniel Agyei golini,   beki wa kulia akiwa Javier Bukungu,  kushoto akicheza Mohamed Hussen beki ya Kati wanaweza kuanza Abdi Banda na Juuko Murshid kiungo namba sita James Kotei Huku kiungo namba nane anaweza kuanza Mzamiru Yassin,  Winga kuna asilimia kubwa ya kuanza Shiza Kichuya kulia na Saidi Ndemla Huku upande wa Mshambuliaji kama Kawaida Laudit Mavugo na Ibrahim Ajibu.. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Simba Sc kumkosa Mkude mechi na Mbao Fc Jumatatu Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top