728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, April 06, 2017

    Simba Sc Nyasi bandia zetu ziko salama kabisa

                                     

    Faridi Miraji , Dar es salaam.                          

    Alhamisi iliyopita kampuni ya udalali ya Majembe Auction Mart ilitangaza Mnada wa kuuza nyasi bandia na magoli ya timu ya Simba Sc.  Hii ilitokea kutokana na timu ya Simba kushidwa kulipa kodi ya Shilingi milioni 80 walizokuwa Wanadaiwa na TRA. 

    -Baada ya Simba kuhaha na kuomba kupewa muda zaidi ili wakomboe Nyasi zao,  TRA waliipa Simba wiki moja wawe wamelipa deni hilo zaidi ya hapo lazima zingepigwa Mnada.  

    Viongoz wa Simba akikaa kikao na kuamua kujichangisha mpaka walipata hizo milioni 80 na Jana ndio ilikuwa siku ya mwisho ya kulipa deni hilo na Simba wakafanya hivyo 

    Makamu wa Rais wa Simba,  Geoffrey Nyange Kaburu na Mkurungezi wa Elimu kwa walipa kodi wa TRA, Richard Kayombo Amedhibitisha hilo 

    “Ni kweli Simba wamelipa pesa waliyokuwa wanadaiwa kwa ajili ya nyasi zilizo hapa bandarini, zimelipwa jana ila wasingelipa mnada ungeendelea kama kawaida maana siku ya mwisho ya kulipa ilikuwa ndio hiyo jana."alisema Richard Kayombo.

    Huku Kaburu alisema wanachosubiri sasa ni kupata oda ya TRA kuwaruhusu kuziondoa nyasi hizo ili sasa walipe gharama za bandari kabla hawajamaliza rasmi zoezi hilo.

    “Tumelipa ushuru jana, tunasubiri ‘release order’ ili sasa tukajue ‘storage’ ni kiasi gani tulipe, baada ya hapo tutaondoka na nyasi zetu tukazihifadhi mahali kusubiri mvua ziishe mchakato wa uwanja uendelee,” alisema Kaburu.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Simba Sc Nyasi bandia zetu ziko salama kabisa Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top