728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, April 07, 2017

    Ngoma,Tambwe na Kamusoka wapona,wako tayari kuwavaa waarabu kesho


    Faridi Miraji , Dar es salaam.                        

    MSHAMBULIAJI Donald Ngoma na kiungo Thabani Kamusoko wameanza kufufua matumaini ya Yanga baada ya kuanza mazoezi mepesi na wenzao . Wazimbabwe hao, waliukosa mchezo uliopita wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Azam FC kutokana na majeraha ya goti yaliyowaweka nje ya uwanja akiwemo na Mrundi, Amissi Tambwe ambaye naye ameanza  mazoezi tayari.


                         

    Daktari Mkuu wa timu hiyo, Edward Bavu, alisema wachezaji wake majeruhi wote wamepona na wameanza mazoezi isipokuwa Justine Zulu  ambae aliyeumia katika mechi ya Azam FC.

    "Ni habari njema kwa mashabiki wa Yanga kusikia wachezaji wetu ambao ni muhimu kwenye timu wakirejea uwanjani katika mechi muhimu ambayo tunahitaji ushindi katika uwanja wetu wa nyumbani."

    Nyota hao, wamerejea uwanjani ikiwa ni siku chache kabla ya mchezo wa kwanza dhidi ya MC Alger ya Algeria watakaovaana Kesho kwenye uwanja wa taifa kwenye mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Ngoma,Tambwe na Kamusoka wapona,wako tayari kuwavaa waarabu kesho Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top