728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, April 07, 2017

    Mzee Bakharesa , Je kiwanda cha Azam FC kitaanza lini Uzalishaji?


    Na Chiki Mchoma, Dar es salaam.               

    Tanzania ya leo ni tamu sana. 

    Siasa imetamalaki... Kila kitu ni Siasa na Siasa ndiyo Maisha. 

    Eti hata Soka nalo lina Siasa zake !! 
    Ingawa sisi tulioonja chumvi kidogo tulisisitizwa kuwa Siasa ni Kilimo. Sijui kama Sera hii ipo tena nadhani imeenda na mwenyewe !! 

    Tanzania ya Viwanda imetangazwa !! 

    Kwa nchi zilizoendelea Viwanda ndio kila kitu katika Mafanikio ya Nchi yenyewe na Wananchi wake kwa Ujumla. 

    Wenye elimu ya kale kidogo tunakumbuka juu ya Mapinduzi ya Viwanda huko Ulaya na Marekani yalivyosababisha upungufu wa Watu wa Kufanya kazi na Kusababisha Wazungu watoke huko kuja kutukusanya Waafrika ili tukafanye kazi kwenye Viwanda vyao. 

    Nadhani Maendeleo ya Nchi za Ulaya na Marekani mnayaona yalivyo kutokana na Ukuaji huo wa Viwanda. 

    Hiyo ndiyo nguvu ya Viwanda... Kila mtu Ulaya yuko Bize na Kazi ili kulijenga Taifa lake na Kuinua hali yake Kiuchumi. 

    Hapa nchini kwetu Tanzania hakuna asiyeijua Familia ya Mzee Said Salim Bakhressa. 

    Kama hukula Mkate wao asubuhi basi utakula andazi lao au chapati yao.. Iwe waliyoandaa wao au kupitia Viwanda vyao au Aliyoandaa Mama au Baba muuzaji aliyetumia Unga wao. 

    "Wana Viwanda Vingi Mno Kiasi Siwezi kuwa na Muda wa Kutosha Kuvielezea Hapa !!."

    *LAKINI KUNA KIWANDA KIMOJA WAMEKITELEKEZA HAWAKITAKI AU HAWATAKI KIZALISHE AU SIJUI LINI KITAANZA UZALISHAJI?? ...Chiki Mchoma bado Najiuliza.*

    *Kiwanda cha Azam FC Kitaanza lini Uzalishaji??.*

    Mwaka 1998 akiwa safarini kuelekea Mji Mkuu wa Uholanzi pale Armstadam, Rob Moore alikuwa na Wazo moja tu la Kumuuza Benni Mc Carthy kwenye Klabu ya Ajax Armstadam. 

    Pembeni yake alikuwa na Kijana huyo Mtulivu na Mpole lakini machachari uwanjani aliyemtoa kwenye Kiwanda chake Kidogo cha kukuza Wachezaji kilichoitwa Seven Stars FC. 

    Baada ya Viongozi wa Ajax Armstadam kuona uwezo Mwanana wa Benni Mc Carthy walijiridhisha kuwa kuna akina Ben wengi nchini Afrika ya Kusini hivyo walimsihi Rob Moore aandae Mazingira mazuri ili wao Ajax Armstadam waje kuweka Kiwanda kikubwa kabisa pale Sauz cha kuzalisha Wachezaji. 

    Ndiyo ile Timu unayoisikia leo inayoitwa Ajax Cape Town. 

    Ambayo mechi yake ya kwanza tu kubwa ilicheza dhidi ya Kaizer Chiefs... Klabu Kongwe kabisa na yenye Mashabiki wengi pale Sauz na Kufanikiwa kuifunga goli moja ambalo limebaki kuwa historia iliyotukuka kwao. 

    Mpaka sasa Ajax Cape Town ina Vituo vya kuibua Vipaji vya Soka ( Academies ) nchini nzima ya Afrika Kusini huku ikiwa na Wachezaji Vijana zaidi ya 8,000. 

    Dar es Salaam na Tanzania nzima hakuna asiyeyajua Mafanikio ya Kibiashara ya Biashara za Familia ya Mzee Said Salim Bakhressa. 

    Lakini ajabu ni kuwa binafsi Bado najiuliza Je, wakati familia hii inakusudia kuanzisha Timu ya Azam FC hawakuhusisha Wataalam wa Biashara ya Soka kama ambavyo kabla ya kuanzisha Viwanda vyao Vingine hupata Taarifa sahihi za kitaalam kuhusu Biashara husika?? 

    Mbona Azam FC ni Kiwanda kikubwa sana lakini chenye Uzalishaji mdogo na Usiokidhi kiu ya Walaji?? 

    Kutokuwapo na Wataalam wa Biashara ya Mpira ndani ya Azam FC ndiko kunakosababisha Viwango vya Soka vya Vijana wetu walioko pale kina Salum Aboubakar 'Sure Boy', Himid Mao 'Ninja' Gabriel Michael, Shaaban Iddy, Ramadhani Singano 'Messi' na wengineo wengi kutofikia Malengo makubwa ya kisoka huku wakiwa na Vipaji vikubwa ambavyo havitakiwi kutumika hapa kwenye mpira wa Maneno mengi. 

    Hakika naamini bila shaka yoyote Uwezo wa Aish Manula sio wa nchi hii... Lakini mbona bado tuko nae na umri unazidi kusogea?? 

    Tatizo kubwa ni hilo... Hakuna Wataalam wa Biashara ya Mpira pale Azam FC.

    Laiti kama wangekuwepo kwa uwekezaji ule wa Familia ya Bakhressa pale Chamazi basi leo hii Kiwanda kile kingeshakuwa kimeleta faida kubwa mno. 

    Binafsi naamini katika Viwanda vyote vya Bakhressa... Pengine kile kinaongoza kwa kuleta hasara kuliko faida. 

    Kwa nn asiwepo Mtaalam atakayekwenda kwenye Vilabu mbali mbali Vikubwa Ulaya na kuinadi Klabu ya Azam na Wachezaji wake?? 

    Kwa nn asiwepo mtu atakayekwenda kuvishawishi Vilabu hivyo kuja kutembelea Azam Complex na Kuona utayari wa Kiwanda kile na Bidhaa nzuri zilizopo pale?? 

    Azam FC ya leo ilitakiwa iwe tayari imeshajiimarisha Dunia nzima. 

    Ajax Cape Town ukiangalia Maendeleo yake ndani ya Miaka kumi 1998 - 2008 utajua kwa nn Azam FC ilitakiwa kuwa Kiwanda kikubwa kuliko kilivyo sasa. 

    Azam kwa sasa ina Miaka Tisa 2008 - 2017 toka iingie Ligi Kuu. 

    Sasa kapige hesabu za Faida na Hasara kwa miaka yote Tisa ndipo utakapogundua kuwa hiki ndicho Kiwanda kinachotia hasara maradufu kuliko kuleta faida iliyokusudiwa. 

    WAHUSIKA AMKENI KABLA HAMJAKIFUNGA KIWANDA HIKI. 

    KIWANDA HIKI KIKITENDEWA HAKI KINA UWEZO WA KULETA FAIDA NA SIFA KUBWA KWA TAIFA KULIKO KIWANDA CHOCHOTE CHA FAMILIA HII NCHINI. 

    IWAPO MAFANIKIO YA KUWA NA VILABU RAFIKI NJE YA NCHI AMBAVYO VITAKUWA VINANUNUA WACHEZAJI AZAM FC BASI NI JIBU TOSHA KUWA MABILIONI YA PESA YATAKUWA YANAINGIA KILA SIKU PALE AZAM COMPLEX.

    KWA NINI WASIAJIRIWE WATAALAMU YA BIASHARA YA MPIRA TOKA NJE?? 

    KWA NINI AZAM FC ISIWE NA URAFIKI NA VILABU VIKUBWA SPAIN, FRANCE, GERMANY, ITALY, ENGLAND, URENO, SAUZ, EGYPT nk.??? 

    KWA NN HAKUNA MASHINDANO MAALUM YA JAPO TIMU KUBWA NNE AFRIKA ZITAKAZOCHEZA PALE AZAM COMPLEX NA MASHINDANO KUONESHWA AFRIKA NZIMA HIVYO TIMU NA WACHEZAJI KUPATA FURSA KUBWA YA KUJULIKANA?? 

    AZAM FC INAWEZA KUZIALIKA WAKATI WA MAANDALIZI YA MSIMU KLABU KAMA ZAMALEK, TP MAZEMBE, MAMELOD SUNDOWNS NA YENYEWE ZIKASHIRIKI MASHINDANO MAALUM YA WIKI MOJA TU. 

    UWEKEZAJI ULIOFANYIKA PALE AZAM COMPLEX UNATOSHA KUZIVUTIA TIMU KUBWA KUJA KUWA RAFIKI NAYO.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Mzee Bakharesa , Je kiwanda cha Azam FC kitaanza lini Uzalishaji? Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top