728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, April 07, 2017

    Zamalek yamnasa kocha wa Porto ya Ureno


    Cairo,Misri.

    KLABU ya Zamalek inayoshiriki ligi kuu ya nchini Misri leo Ijumaa imemtangaza Mreno Augusto Inacio kuwa kocha wake mkuu mpya.

    Inacio mwenye umri wa miaka 67 ameingia kandarasi ya mwaka mmoja na nusu ya kuifundisha miamba hiyo ya jiji la Cairo akichukua mikoba ya mzawa,Mohamed Helmy aliyetimuliwa kibarua hicho hivi karibuni kutokana na muendelezo wa matokeo mabovu.

    Akifanya mahojiano mara baada ya kusaini kandarasi hiyo,Inacio amesema atafanya kila awezalo kuipa mafanikio makubwa klabu hiyo.

    Kabla ya kutua Zamalek, Inacio aliwahi kuvifundisha vilabu vya Rio Ave, Marítimo,Sporting CP na Moreirense vya nyumbani kwao Ureno.Pia aliwahi kuifundisha klabu vya Al Ahli SC ya nchini Qatar.

    Msimu uliopita ulikuwa ni wenye mafanikio zaidi kwa Inacio kwani akiwa kocha msaidizi wa Porto aliweza kutwaa ubingwa wa Taça da Liga (Kombe la Ligi) baada ya kuifunga Braga kwenye mchezo wa fainali.

    Jumla Inacio ameshinda vikombe vitatu akiwa kocha mkuu na vikombe vinane akiwa kocha msaidizi.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Zamalek yamnasa kocha wa Porto ya Ureno Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top