728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, April 08, 2017

    Balotelli azidi kutakata ligue 1


    Nice, Ufaransa.

    Usiku wa jana mshambuliaji mtukutu toka Italia anaekipiga na Nice FC , aliipa ushindi timu yake akipiga mbao mbili za maana dhidi ya Lile.

    Goli la kwanza la Baloteli alipiga dakika ya 17 akiua mtego wa kuotea wa Lile kwa shambulio zuri la kushitukiza . Hii ilikuwa baada ya Amadou wa Lile kutikisa nyavu za Nice kunako dakika ya 14 hivyo ilimchukua dakika tatu ! tu Mario Baloteli kuwasazishia Nice. 


    Dakika moja kabla ya muda wa mapumziko , Baloteli tena aliwatungua Lile kwa ' tapping ' nzuri akiwaacha hoi walinzi wa Lile. 

    Magoli haya mawili ya Baloteli , ndio magoli pekee aliyofunga msimu huu nje ya uwanja wao wa nyumbani lakini akiwa na consistency nzuri ya kutikisa nyavu mfululizo katika mechi tano. 

    Mpaka sasa mshambuliaji huyu katika mechi 19 alizoichezea Nice msimu huu akianza mechi 17 , ametikisa nyavu mara 13. Ana kadi 5 za njano na 2 nyekudu. 

    Ushindi wa Nice jana umeipeleka OCG Nice nafasi ya pili katika ligi ikiwa na alama 70 ikizidiwa alama 1 na Monaco wenye alama 71. Nice wamecheza mechi 32 lakini Monaco wamecheza mechi 30 . 


    Nice amemshusha PSG mwenye alama 68 baada ya kucheza mechi 30 . Mechi ijayo wanakutana na vinara Monaco . 

    Benchi la ufundi la OCG Nice bado lina imani kubwa na kipaji cha Baloteli na nidhamu yake kwa sasa .




    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Balotelli azidi kutakata ligue 1 Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top