728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, June 18, 2016

    SIMBA SC YAENDELEA KUIGEUZA MTIBWA SUGAR SHAMBA LA BIBI,YACHOMOA TENA MMOJA,ITAKUWA IKIMLIPA 250,000 KILA INAPOSHINDA MCHEZO

    Dar es Salaam,Tanzania.

    SIMBA SC imeendelea kujichukulia wachezaji toka Mtibwa Sugar ya Manungu,Morogoro baada ya kufanikiwa kumsajili aliyekuwa kiungo wake wa ushambuliaji,Mohammed Ibrahim pichani. 

    Ibrahim amesaini mkataba wa miaka miwili wenye sharti la kulipwa Sh 250,000 kama posho yake kila timu inaposhinda,” amesema mmoja wa viongozi wa Kamati ya Usajili ya Simba SC.Ada ya uhamisho huo imefichwa.

    Ibrahim anakuwa mchezaji wa pili kujiunga na Simba SC akitokea Mtibwa Sugar katika kipindi kisichozidi wiki moja.Wa kwanza ni Muzamil Yasin ambaye pia nae amesaini mkataba wa miaka miwili.

    Mpaka sasa Simba SC imeshawanasa nyota wanne tangu kufungwa kwa pazia la Ligi Kuu Bara wakiwemo Peter Semwanza na Jamal Mnyate wote toka Mwadui FC.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: SIMBA SC YAENDELEA KUIGEUZA MTIBWA SUGAR SHAMBA LA BIBI,YACHOMOA TENA MMOJA,ITAKUWA IKIMLIPA 250,000 KILA INAPOSHINDA MCHEZO Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top