Valencia,Hispania.
Raisi wa klabu ya Valencia Amadeo Salvo ameamua kuvunja ukimya juu ya ya hatima ya mlinzi wa klabu hiyo Muargentina Nicolas Otamendi anayewindwa vikali na klabu ya Manchester United.
Amadeo amesema klabu hiyo yenye makazi yake katika dimba la Mestalla itakuwa tayari kumuuza mlinzi huyo mahiri wa kati ikiwa tu klabu ya Manchester United itakuja na kitita cha €50m.
Kauli hiyo imekuja zikiwa zimepita siku chache tangu wakala wa Otamendi,Eugenio Lopez aseme mteja wake anataka kutimka Valencia na kwenda kukipiga kwingineko.
Wakati huohuo,kutoka Gazeti la Gazetta cello spoti la Italia habari zinasema kiungo Sami Khedira atakuwa katika jiji la Torino leo au kesho kwa ajili ya kufanyia vipimo na hatimaye kusaini kuichezea klabu ya Juventus.
0 comments:
Post a Comment