728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, May 30, 2015

    MAN UNITED YAMTAKA BACCA,ARSENAL YASAJILI WAWILI KWA MPIGO

    Tetesi na Paul Manjale.

    Arsenal:Klabu ya Arsenal imeanza mbio za usajili mpya baada ya kusajili nyota wawili makinda toka klabu ya RC Lens kwa £3m.Makinda hao ambao pia walikuwa wakiwindwa na Manchester United ni Yassin Fortune 16 kiungo wa kati na Jeff Reine-Adelaide 17 anayecheza nafasi ya ushambuliaji.

    Clyne:Klabu ya Southampton imeiambia klabu ya Liverpool kutoa kitita cha £15m baada ya kukataa ofa ya kwanza ya £10m kwa ajili ya mlinzi wake wa kulia Nathaniel Clyne

    Christensen:Klabu ya Liverpool iko mbio kutoa kitita cha £6m ili kumsajili mlinzi kinda wa klabu ya Chelsea Andreas Christensen ambaye pia anawindwa na vilabu vya Ac Milan pamoja Borrussia Monchengladibach.

    Bacca:Klabu ya Manchester United imeripotiwa kujiingiza katika mbio za kumsajili mshambuliaji hatari wa klabu ya Sevilla Bacca kwa kitita cha £21.3m

    Cuadrado:Klabu ya Inter Milan kupitia kwa kocha wake mkuu Roberto Mancini inapanga kumsajili winga wa klabu ya Chelsea Juan Cuadrado.Inter imeripotiwa iko tayari kutoa kitita cha £26m ili kumrejesha tena Italia nyota huyo.

    Rodriguez:Klabu ya Arsenal imeanza kumtupia jicho mlinzi wa kushoto wa klabu ya Wolfsburg Ricardo Rodriguez 22 kwa ajili ya kuchukua nafasi ya mlinzi Nacho Monreal anayewindwa na klabu ya Atletico Bilbao ya kwao Hispania.Rodriguez ana thamani ya £21m

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MAN UNITED YAMTAKA BACCA,ARSENAL YASAJILI WAWILI KWA MPIGO Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top