Sevilla,Hispania.
Mabao mawili yaliyofungwa na mshambuliaji hatari Carlos Bacca jana usiku yalitosha kuipa Sevilla Kombe la Europa ligi mbele ya klabu ya Ukraine FC Dnipro Dnipropetrovsk kwa bao 3-2 katika mchezo wa fainali uliyochezwa katika dimba la National Stadium huko Warsaw,Poland.
Sevilla inaweka historia ya kuwa klabu ya kwanza kutwaa taji hilo mara nne.Sevilla ilitwaa taji hilo mara ya kwanza mwaka 2006, 2007,2014 na 2015.
Kufuatia ushindi huo wa jana usiku Sevilla inajipatia tiketi ya kushiriki ligi ya mabingwa msimu ujao baada ya sheria mpya ya UEFA kuagizwa hivyo kwa bingwa wa ligi ya Europa.
Kufuatia Sevilla kupata nafasi hiyo nchi ya Hispania itawakilishwa na vilabu vitano katika ligi ya mabingwa ambavyo ni Real Madrid,Barcelona,Atletico Madrid,Valencia na Sevilla.
0 comments:
Post a Comment