728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, May 27, 2015

    USAJILI:LIVERPOOL YAMFATA KONDOGBIA,UNITED YAMZIMIKIA DANTE

    Tetesi na Paul Manjale.

    Kondogbia:Klabu ya Liverpool imeanza kujipanga kwa ajili ya msimu ujao wa ligi baada ya kuripotiwa kutuma mwakili wake katika klabu ya Monaco kwa ajili ya kuwanasa nyota Geoffrey Kondogbia na Aymen Abdennour.Ikiwa dili hilo litakubalika Liverpool italazimika kutoa kitita cha £50m.

    Dante:Klabu ya Manchester United imeripotiwa kumtolea macho mlinzi wa Bayern Munich Mbrazil Dante Bonfim Costa Santo 31baada ya kuendelea kupata ugumu katika usajili wa walinzi Matt Hummels na Nicolas Otamendi

    Pirlo:Kiungo aliyembioni kuikacha klabu ya Juventus Andrea Pirlo ameripotiwa kuvichunia vilabu vya Chelsea na Liverpool na badala yake atajiunga na klabu ya New York City Fc inayoshiriki ligi ya Marekani MLS

    Kolo:Klabu ya Liverpool imemuongeza makataba wa mwaka mmoja mlinzi wake Kolo Toure huku pia ikimpa ulaji mwingine wa miaka minne kinda wake Andre Wisdom.

    Moreno:Klabu ya Arsenal imeripotiwa kujiandaa kupiga hodi katika klabu ya Villarreal kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji Muhispania Gerrard Moreno (23) kwa ada ya £3m.Moreno amefunga jumla ya magoli 16 katika michezo 36.

    Adebayor:Klabu ya Aston Villa kupitia kwa kocha wake Tim Sherwood inapanga kumsajili mchezaji asiye na furaha katika klabu ya Tottenham Emanuel Adebayor kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: USAJILI:LIVERPOOL YAMFATA KONDOGBIA,UNITED YAMZIMIKIA DANTE Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top