Kovacic:Klabu ya Liverpool imeripotiwa kuitaka saini ya nyota wa Inter Milan Mateo Kovacic kwa ada ya €18m ili kuimarisha safu yake ya kiungo.
Gundogan:Klabu ya Bayern Munich imeripotiwa kuandaa mshahara wa €8m kwa mwaka na mkataba wa miaka mitatu kwa kiungo wa Borussia Dortmund Illikay Gundogan.
Ancellotti:Kutoka Italia habari zinasema klabu ya Ac Milan inajiandaa kuachana na kocha wake wa sasa Felipe Inzagi na kumuajiri Carlo Ancellotti.Milan imeandaa €86m kwa ajili ya kusuka upya kikosi chake.
Gueye:Klabu ya Southampton imeripotiwa kuwa katika mazungumzo na klabu ya Lille kwa ajili ya kumsajili kiungo Idrissa Gueye kwa ada ya €10m ili kuziba pengo la kiungo wake Morgan Schneiderlin anayetarajiwa kutimka katika kipindi hiki cha usajili barani Ulaya.
Upamecano:Klabu ya Manchester United imeshinda mbio za kumuwania kinda wa kifaransa toka klabu ya Valenciennes Dayot Upamecano (16).Ili kukamilisha dili hilo United italazimika kulipa kitita cha €450,000.
0 comments:
Post a Comment