Tetesi na Paul Manjale
Arsenal:Klabu ya Arsenal imeongeza jina la mshambuliaji wa Dortmund Pierre-Emerick
Aubameyang mwenye thamani ya £29.9m kama mbadala iwapo itashindwa kumsajili nyota wa Porto Jackson Martinez
Koscienly:Klabu ya Arsenal imeripotiwa kutaka kumtoa mlinzi wake Laurent Koscielny kama chambo ili kumpata mshambuliaji wa Real Madrid Karim Benzema.
Navas:Klabu ya Liverpool imeripotiwa kuitaka saini ya mlinda mlango wa klabu ya Real Madrid Keylor Navas baada ya kuchoshwa na kiwango duni cha mlinda mlango wake Simon Mignolet.Liverpool imetenga £10m
Milner:Klabu ya Manchester United kupitia kwa mwenyekiti wake Ed Woodward imeripotiwa kuulizia uwezekano wa kumsajili kiungo wa Manchester City anayemaliza mkataba wake hivi karibuni James Milner.
Evans:Klabu ya Everton imeishtuwa klabu ya Manchester United baada ya kutangaza kumtaka mlinzi Jonny Evans ambaye amebakiza mwaka mmoja pekee katika mkataba wake wa sasa.Thamani yake ni £5m
Lloris:Mlinda mlango Hugo Lloris ameiambia klabu yake ya Tottenham kuwa anataka kucheza michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya.Hii imekuja siku chache tu baada ya klabu ya Manchester United kuhusishwa kutaka kumsajili nyota huyo wa zamani wa klabu ya Lyon.
0 comments:
Post a Comment