London,England.
Wachezaji watatu wa timu ya Leicester City ya Ligi Kuu ya England ambao wanadaiwa kuonekana katika mkada wa video wakionyesha vitendo vya ubaguzi wa kimapenzi wameomba radhi kutokana na tabia yao hiyo.
Picha ambazo zimekuwa zikiwaonyesha wachezaji Tom Hopper, Adam Smith na James Pearson - mtoto wa kocha Nigel Pearson -walionekana katika gazeti la Sunday Mirror.
Mmoja wa wanaume hao katika video hiyo,ambayo ilipigwa nchini Thailand, anasikika kutoa lugha ya matusi ya kibaguzi dhidi ya mwanamke mmoja.Klabu ya Leicester imesema itaendessha mchakato wa kawaida wa uchunguzi wa kitendo hicho.
Taarifa ya klabu hiyo imenukuliwa ikisema bodi ya Leicester imesikitishwa sana na tukio hilo ambalo limewahusisha vijana wao watatu weledi wa soka wakati wa safari yao ya hivi karibuni nchini Thailand.
Tom Hopper, James Pearson na Adam Smith wangependa kuomba radhi kutokana na tabia yao kwa wanawake waliohusika katika tukio hilo, kwa klabu yao na wamiliki wake, kwa wapenzi na mashabiki wa timu ya Leicester na kwa familia zao.
Timu hiyo ya Ligi Kuu ya England ilikuwa nchini Thailand nyumbani kwa wamiliki wa timu hiyo baba na mwana Vichai na Aiyawatt Srivaddhana timu ya Cityprabha.
0 comments:
Post a Comment