Soares:Klabu ya Arsenal imeripotiwa kumtaka mlinzi wa klabu ya Sporting Lisbon ya Ureno Cedric Soares kwa ada ya £5m
Schneiderlin:Klabu ya Manchester United imeripotiwa kukalia kiti cha uongozi katika mbio za kumsajili kiungo wa Southampton Morgan Schneiderlin kwa ada ya £25m.
Liverpool:Klabu ya Liverpool iko mbio kukamilisha usajili wa nyota wanne kwa ajili ya kuongeza nguvu katika kikosi chake.Nyota wanaowindwa ni Christian Benteke,Nathaniel Clyne,James Milner na Danny Ings.
Costa:Mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa ameripotiwa kutaka kurudi katika klabu yake ya Atletico Madrid kufuatia kuchoshwa na maisha ya England hasa chakula,lugha na hali ya hewa.
Reina:Kocha Raphael Benitez ameonyesha nia ya kumtaka mlinda mlango Pepe Reina kama chaguo la pili katika klabu ya Real Madrid.
0 comments:
Post a Comment