728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, May 26, 2015

    USAJILI:MADRID KUFANYA KUFURU KWA AGUERO,ANCELOTTI HUYO WESTHAM

    Paul Manjale.

    Sterling:Klabu ya Manchester City iko tayari kutoa kitita cha £43m pamoja na mshambuliaji wake Stevan Jovetic kwa ajili ya kumsajili nyota wa Liverpool  Raheem Sterling.

    Di Maria:Klabu ya PSG bado haijakata tamaa ya kuinasa saini ya winga wa klabu ya Manchester United Angel Di Maria.Kupitia vyombo mbalimbali vya habari taarifa zinadai mwenyekiti wa PSG Nasser al-Khelaïfi yuko tayari kumtoa mlinzi wake wa kulia  Gregory van der Wiel na pesa ili kukamilisha dili hilo.

    Walcott:Klabu ya Liverpool imeripotiwa kuvutiwa zaidi na dili la kubadirishana wachezaji kati yake na Arsenal baada ya nyota wake Raheem Sterling kuonyesha wazi kuitaka Arsenal badala ya Manchester City.Liverpool imeona dawa sahihi na kumtaka Theo Walcott na wao kumuachia Sterling.

    Ancelloti:Klabu ya West ham imeripotiwa kuanza mipango ya kumfukuzia kocha Carlo Ancelloti ili kuja kuchukua nafasi ya kocha wake wa sasa anayetimka klabuni hapo Sam Allardyce.

    Aguero:Klabu ya Real Madrid imeripotiwa kuwa tayari kutoa kitita cha £63.9m kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji matata wa klabu ya Manchester City Kun Aguero kwa ajili ya kukiimarisha kikosi hicho.

    Van Persie:Kocha wa zamani wa klabu ya Swansea City Michael Laudrup ambaye kwa sasa anaionoa klabu ya Lekhwiya ya Qatar amemtaka mshambuliaji wa klabu ya Manchester United Robin Van Persie kujiunga na klabu hiyo ya falme za kiarabu. 


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: USAJILI:MADRID KUFANYA KUFURU KWA AGUERO,ANCELOTTI HUYO WESTHAM Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top