728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, May 26, 2015

    SAMATTA KIBOKO AONYESHA JEURI YA FEDHA

    Dar es salaam,Tanzania.

    Samatta anayekipiga katika klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo,anatajwa kuwa mmoja wa wachezaji watanzania wanaoingiza fedha nyingi kupitia soka – akiripotiwa kulipwa mshahara usiopungua $8000 kwa mwezi bila kuongeza marupurupu.

    Mmoja ya wachezaji wa kitanzania wenye mafanikio katika soka nje ya mipaka ya Tanzania, Mbwana Samatta leo asubuhi ameposti picha ya gari lake jipya analotumia akiwa nchini Tanzania.

    Gari aliloposti Samatta ni Range Rover lenye rangi ya damu ya mzee ambalo lina namba za usajili za Tanzania na linakua gari la pili la thamani ambalo Samatta ameliweka hadharani baada ya mwaka 2013 kulionyesha gari lake aina ya Chrysler Crossfire ambalo lilikuwa na thamani ya takribani millioni 50 za kitanzania.

    Samatta alijiunga na TP Mazembe akitokea Simba SC kwa ada ya uhamisho iliyovunja rekodi kwa kipindi hicho ya $100,000.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: SAMATTA KIBOKO AONYESHA JEURI YA FEDHA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top